Ikiwa ni wiki 2 tu zimepita baada ya bibi aliyedhaniwa kuwa mchawi
(80) kukutwa nje ya nyumba ya mtu akiwa uchi hajitambui katika mtaa wa
Mageuzi kata ya Ndembeza mjini Shinyanga,matukio yanayohusishwa na imani
za kishirikina yameendelea kuacha watu midomo wazi ambapo leo asubuhi
binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23- 25 aliyedaiwa kuwa mchawi
amekutwa hajitambui akiwa amevaa nguo nyeusi,kashikilia chungu kidogo
kwenye mlango wa nyumba ya mtu katika mtaa wa Bushushu kata ya Lubaga
katika manispaa ya Shinyanga huku akidai kuwa amefika mahali hapo kwa
kutumia chungu
Wakazi
wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio nje ya nyumba aliponasa binti huyo
anayedhaniwa kuwa mchawi kutokana na nguo alizovaa na dawa nyeusi
alizopaka kwenye mwili wake.Binti huyo kwamba alifika mahali hapo na
wenzake kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa
ya Massawe aliyegoma kuoa ndugu yao na badala yake akaoa mwanamke
mwingine.
Tukio hili limetokea leo asubuhi katika mtaa
wa Bushushu nyumbani kwa Robinson Massawe ambapo binti huyo alikutwa
amelala mbele ya mlango wa nyumba hiyo akiwa hajitambui na baada ya
kusemeshwa ndipo akasimulia yaliyomkuta kwamba alifika mahali hapo na
wenzake zaidi ya 10 kutoka kanda ya ziwa kufanya sherehe baada ya
kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya Massawe ili ndugu yao aolewe
na baba wa familia hiyo.Kwa mujibu wa ndugu wa baba mwenye nyumba
wameiambia Malunde1 blog kuwa kweli ndoa hiyo ilivunjika tangu tarehe
17.9.2014
Pichani
binti aliyejitambulisha kwa jina la Coletha akiwa amevaa kishirikina
huku mwili wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi akidai kuwa alikuwa
anaongoza wenzake zaidi ya 10 Geita,Mwanza na Shinyanga kuwanga katika
nyumba hiyo.Baada ya kukutwa hapo mlangoni wakazi wa eneo hilo walifika
eneo la tukio kisha mwenyekiti wa mtaa huo Ruben Masanja akimwomba
mwenye nyumba amruhusu binti aingie ndani kwa usalama wake
Mguu wa binti huyo aliyedai kutoka Ushirombo ukiwa umepakwa dawa nyeusi pamoja na usoni,mikononi na mgongoni.
Binti
huyo amesema leo ni mara ya tatu wanakuja kufanya uchawi wao,lengo lao
ni kutaka ndugu yao aolewe na Massawe,walikuja siku ya kwanza wakakuta
mke wa Massawe akisali,wakashindwa,wakarudi kwa mara ya pili kwa ajili
ya kusambaratisha ndoa,wakafanikiwa, leo yeye alikuwa kiongozi wa
wachawi wengine walikuja kufanya sherehe kwa kazi nzuri waliyoifanya
lakini wenzake wamemkimbia-
Wakazi wa Shinyanga wakichungulia kwenye madirisha kuona kinachoendelea ndani
ambapo
baada ya kumhoji binti huyo alisema alifika kwenye familia hiyo,akiwa
kiongozi wa kundi la wachawi zaidi ya 10 kutoka Ushirombo,Misungwi na
Shinyanga wakitumia vyungu na ungo majira ya saa 9 usiku kwa ajili ya
kufanya sherehe baada ya kufanikiwa kusambaratisha kichawi ndoa ya
Massawe na Mary Joseph.
Askari
polisi kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wanaotumia pikipiki
kuzunguka maeneo mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga wakijadili
jambo ndani ya nyumba alimohifadhiwa binti huyo
Askari polisi wakimlinda Binti huyo asipigwe na wananchi waliofika eneo la tukio
Wananchi wakisubiri mchawi atoke ndani ya nyumba,,Aaskari polisi akimtoa ndani ya nyumba binti huyo ili kumpandisha kwenye gari la polisi
Binti akiondolewa eneo la tukio
Binti akiwa ndani ya gari la polisi
Gari la polisi likiondoka eneo la tukio
Wakazi wa Shinyanga wakiondoka eneo la tukio-
0 comments:
Post a Comment