Latest News

Showing posts with label udaku. Show all posts
Showing posts with label udaku. Show all posts
Ikiwa ni wiki 2 tu zimepita baada ya bibi aliyedhaniwa kuwa mchawi (80) kukutwa nje ya nyumba ya mtu akiwa uchi hajitambui katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembeza mjini Shinyanga,matukio yanayohusishwa na imani za kishirikina yameendelea kuacha watu midomo wazi ambapo  leo asubuhi binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23- 25 aliyedaiwa kuwa mchawi amekutwa hajitambui akiwa amevaa nguo nyeusi,kashikilia chungu kidogo kwenye mlango wa nyumba ya mtu katika mtaa wa Bushushu kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga huku akidai kuwa amefika mahali hapo kwa kutumia chungu

 Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio nje ya nyumba aliponasa binti huyo anayedhaniwa kuwa mchawi kutokana na nguo alizovaa na dawa nyeusi alizopaka kwenye mwili wake.Binti huyo kwamba alifika mahali hapo na wenzake kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya Massawe aliyegoma kuoa ndugu yao na badala yake akaoa mwanamke mwingine.
 Tukio hili limetokea leo asubuhi katika mtaa wa Bushushu nyumbani kwa Robinson Massawe ambapo binti huyo alikutwa amelala mbele ya mlango wa nyumba hiyo akiwa hajitambui na baada ya kusemeshwa ndipo akasimulia yaliyomkuta kwamba alifika mahali hapo na wenzake zaidi ya 10 kutoka kanda ya ziwa kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao wa kuharibu ndoa ya Massawe ili ndugu yao aolewe na baba wa familia hiyo.Kwa mujibu wa ndugu wa baba mwenye nyumba wameiambia Malunde1 blog kuwa kweli ndoa hiyo ilivunjika tangu tarehe 17.9.2014

Pichani binti aliyejitambulisha kwa jina la Coletha akiwa amevaa kishirikina huku mwili wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi akidai  kuwa alikuwa anaongoza wenzake zaidi ya 10 Geita,Mwanza na Shinyanga kuwanga katika nyumba hiyo.Baada ya kukutwa hapo mlangoni wakazi wa eneo hilo walifika eneo la tukio kisha mwenyekiti wa mtaa huo Ruben Masanja akimwomba mwenye nyumba amruhusu binti aingie ndani kwa usalama wake

Mguu wa binti huyo aliyedai kutoka Ushirombo ukiwa umepakwa dawa nyeusi pamoja na usoni,mikononi na mgongoni.
Binti huyo amesema leo ni mara ya tatu wanakuja kufanya uchawi wao,lengo lao ni kutaka ndugu yao aolewe na Massawe,walikuja siku ya kwanza wakakuta mke wa Massawe akisali,wakashindwa,wakarudi kwa mara ya pili kwa ajili ya kusambaratisha ndoa,wakafanikiwa, leo yeye alikuwa kiongozi wa wachawi wengine walikuja kufanya sherehe kwa kazi nzuri waliyoifanya lakini wenzake wamemkimbia-


Wakazi wa Shinyanga wakichungulia kwenye madirisha kuona kinachoendelea ndani


ambapo baada ya kumhoji binti huyo alisema alifika kwenye familia hiyo,akiwa kiongozi wa kundi la wachawi zaidi ya 10 kutoka Ushirombo,Misungwi na Shinyanga wakitumia vyungu na ungo majira ya saa 9 usiku kwa ajili ya kufanya sherehe baada ya kufanikiwa kusambaratisha kichawi ndoa ya Massawe na Mary Joseph.

 Askari polisi  kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga wanaotumia pikipiki kuzunguka maeneo mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga wakijadili jambo ndani ya nyumba alimohifadhiwa binti huyo

 Askari polisi wakimlinda Binti huyo asipigwe na wananchi waliofika eneo la tukio

Wananchi wakisubiri mchawi atoke ndani ya nyumba,,Aaskari polisi akimtoa ndani ya nyumba binti huyo ili kumpandisha kwenye gari la polisi
 Binti akiondolewa eneo la tukio
 Binti akiwa ndani ya gari la polisi
 Gari la polisi likiondoka eneo la tukio
Wakazi wa Shinyanga wakiondoka eneo la tukio-



Wanayoyajua mapenzi wanasema,,,Wapenzi wanapokuwa mahali pamoja ni sawa na watoto tu maana mambo wanayoyafanya huwa katika hali ya kawaida na watu wazima wenye akili zao hawawezi kufanya ila tu kwasababu ya kupenda basi inatufanya tujisikie furaha na wale tunaokuwa nao..
Naili ufurahie haya Mapenzi basi huna budi kufurahi na mpemzi wako na kuwa kama mtoto bila kujali ni nini au utaonekanaje cha msingi ni kumfurahisha yule unaye mpenda..Nakulinda penzi lako


Baada ya kupotea kwa muda mrefu, staa wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi hatimaye ameibuka na kueleza sababu za ukimya wake.

Akizungumza na mwandishi wetu katika mahojiano, Snura amefunguka kwamba ukimya wake ulitokana na kwenda Afrika Kusini ‘Sauz’ kushuti video ya wimbo wake wa Najidabua na siyo kweli kwamba alikuwa mkoani Mbeya kwa mwanaume.
Katika intavyu hiyo, Snura alikanusha tetesi za kuzaa mtoto wa pili na kusisitiza ana mtoto mmoja na wanaosema maneno hayo wamekosa la kusema. 

mwandishi wetu: Huoni kukaa kwako kimya mashabiki wamekusahau?Snura: Hawajanisahau kabisa na hilo nililithibitisha hivi karibuni kwenye shoo niliyofanya Msasani Club (Dar), ambapo walijaa tofauti na mwanzo japokuwa mwanzoni kabla ya shoo nilikuwa nawaza wamenisahau.

Walifurahi sana kwani kwa sasa nimekuja na staili tofauti ya kukata mauno ambayo inatambulika kwa jina la Mauno ya Panya Road, yaani haya ni hatari.

mwandishi wetu: Kuna habari kwamba wewe na mpenzi wako DJ Hunter wa Mbeya mmeachana, hili likoje?

Snura: Unajua katika maisha yangu Hunter ndiye mwanaume wa kwanza kumuanika na sikuwahi kuanika mapenzi yangu kabisa kabla ya hapo. Sasa baada ya kuwa tunatupia picha mbalimbali kwenye mitandao watu walinifuata na kunieleza kwamba ninavyofanya siyo vizuri.
Nilichukua ushauri wao na kuufanyia kazi na mpenzi wangu nikamwambia, tukaacha tabia hiyo. Hali hiyo ya kutokuweka picha ndiyo iliyozusha maneno kibao kwamba tumeachana lakini siyo kweli.

Mwandishi wetu: Hivi huoni kwamba Shilole amekufunika kwa sasa wakati wewe ulikuwa juu zaidi yake?
Snura: Hicho kitu hakipo na Shilole hawezi kunifunika kwani najua kwamba siku zote mbuyu hauwezi kugeuka mchicha.